Wabunge nchini Ujerumani wamepiga kura na kuidhinisha, kwa wingi wa kura, sheria ya kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja, ambapo jumla ya Wabunge 623 wameshiriki zoezi hilo, na kati yao wamepiga kura 393 za ndiyo na 226 za hapana.

Hayo yamejiri siku chache baada ya Kansela Angela Merkel kuondoa upinzani wake dhidi ya mpango huo, lakini kansela huyo, ambaye alionekana kuunga mkono kufanyika kwa kura hiyo Jumatatu, alipiga kura ya kupinga.

Wabunge hao wameidhinisha sheria hiyo ambapo sasa wapenzi wa jinsia moja watakuwa na hadhi ya ndoa kamili na wana haki ya kuasili watoto tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Wapinzani wa Bi Merkel kisiasa walikuwa wanaunga mkono sana hatua hiyo.

Kwa maana hiyo. sheria nchini Ujerumani sasa itasoma: “Ndoa inafanikishwa na watu wawili wa jinsia tofauti au jinsia moja,”

Young Killer Ampa Nay wa Mitego Masharti ili Waende Sawa
?Live: Rais Magufuli akizindua rasmi maonyesho ya Sabasaba