Matumizi ya simu za mkononi hupelekea mtu unayekuwa karibu naye kimwili kuwa  mbali nawe kiakili na mawazo ambayo ameyaelekeza kwa mtu anayewasiliana naye muda huo. Balaa zaidi ni ‘kuchat’ ambapo mtumiaji wa simu hupelekea hisia zake zote kwenye vidole vinavyoandika huku akimuacha aliyenaye akiwa mpweke.

Hii imemgharimu bibi harusi aliyekesha akipokea salamu za pongezi kwenye simu na kumsahau mumewe. Fuatilia kisa hiki…!

Mwanaume mmoja ameamua kumtalakisha mkewe saa chache baada ya kufunga ndoa, kwasababu mkewe huyo mpya alitumia usiku wao wote wa ‘fungate’ kuchat na rafiki zake.

Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan la Saudi Arabia, bibi harusi huyo alikuwa busy akipokea salamu za pongezi kutoka kwa rafiki yake akimsahau mumewe aliyenaye chumbani muda huo.

“Bwana harusi alijaribu kusogea karibu naye na kimahusiano, lakini alishitushwa kuona mkewe anampotezea, hajibu anachoulizwa au hata kuonesha vitendo,” ndugu wa Bwana harusi aliiambia Al Watan.

“Mwanaume alipomuuliza kama rafiki zake ni muhimu kuliko yeye, alimjibu ndio,” walisimulia mkasa walioelezwa na bwana harusi.

Mahakama ya mwanzo katika eneo hilo imejaribu kuwasuluhisha ili waendelee na ndoa yao, lakini mwanaume ameendelea kushikilia msimamo wake wa talaka.

Lowassa, Sumaye watajwa sakata la uuzwaji nyumba za serikali, Mbowe alipua
TFF Bado Wanazongwa Na Jinamizi La Mabadiliko Ya Ratiba

Comments

comments