Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ammy Ninje, amesema kuwa wao kama benchi la ufundi hawatojali kuhusu watu wanaokosoa mbinu za ufundishaji kwasababu hawezi kufanya jambo ili kumfurahisha kila mtu.

Ameyasema hayo leo Mei 11, 2018 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelezea mchezo wa kufuzu mashindano ya kombe la mataifa Afrika chini ya miaka 20 kati ya timu ya Tanzania dhidi ya Mali na kuongeza kuwa kauli za kumpinga au kumpongeza haziwezi kumnyima usingizi.

“Mimi katika maisha yangu sihitaji kujulikana, kwahiyo mtu anikubali au asinikubali hiyo haina maana yoyote  kwangu hayo ndiyo maisha yangu, mimi ninachofanya ni kuwasaidia hawa vijana waendelee katika maisha yao ya mpira, kwahiyo watakao nisapoti au wasionisapoti hawezi kunifanya nisilale usiku,”amesema Ninje

Amesema kuwa timu yake imejiandaa kushinda mchezo huo na kuongeza kuwa timu itatumia mfumo wa kushambulia zaidi ingawa itabidi waweke nidhamu ya ulinzi ili kutoruhusu goli.

Hata hivyo, Mei 13, 2018, timu ya Tanzania itacheza mchezo dhidi ya Mali katika Uwanja wa Taifa, Dar es salaam katika mchezo wa kufuzu mashindano ya kombe la mataifa Afrika chini ya miaka 20 yatakayofanyika nchini Niger February 24, 2019.

Video: DC Karatu azindua duka la kisasa la Kampuni ya simu ya Airtel
Video: Kamanda Mambosasa amshukuru 'Mange' kurudi kundini

Comments

comments