Msanii wa kizazi kipya Christian Bella leo ameachia wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la Punguza kidogo.

Katika kuonesha uweza wa sauti, Bella amefanya kibao hiko bila ya kumshirikisha msanii yeyote ndani na nje ya Africa, Christian Bella ameamua kwenda na kasi ya wasanii washindani Bongo ambao ngoma zao bado zinafanya vizuri na kuvuja rekodi ya kuwa ngoma zilizoangaliwa na watu wengi ndani ya muda mchache.

Ngoma ya Alikiba ‘’seduce me’’ kwa muda wa wiki mbili bado imeendelea kufanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza Tanzania katika mtandao wa Youtube. Huku Zilipendwa ya WCB bado ikiendelea kushika nafasi ya pili.

Tazama hapa chini video ya wimbo huo ikiwa imetayarishwa na Hanscana na kufanywa hapa hapa Bongo, masaa manne yaliyopita ngoma hiyo kwa mara ya kwanza kuruka hewani na kupata watazamaji 4690, Kusapoti muziki wa Bella tazama ngoma hiyo hapa hapa Dar24.

Wananchi wateketeza mali za familia 6 kwa tuhuma za ushirikina
Video: G Van atikisa na 'Kwako', Itazame hapa