Drake amechochea vita ya maneno kati yake na Bosi wa lebo ya Good Music, Kanye West baada ya kusikika akimkejeli alipokuwa akiwasha moto wa mistari jukwaani, Chicago nchini Marekani.

Wakati anaimba wimbo wake ‘Know Yoursef’, Drake alibadili baadhi ya mistari na kuonekana kukejeli mauzo ya albam ya Kanye West iliyobatizwa jina la ‘Ye’.

Kwenye mistari ya wimbo huo badala ya kusikika akisema Kanye alishusha (dropped) mzigo (polos&backpacks), alisema Kanye aliporomoka (flopped).

Drake alionekana kushusha kombora la chumvi kwenye kidonda cha Kanye West ambaye bado anaugulia kuuza nakala 208,000 pekee katika wiki yake ya kwanza kwenye soko la Marekani.

Hata hivyo, mwenzake Drake anasherehekea mavuno ya mauzo manono ya albam yake ‘Scorpion’ ambayo iliuza nakala 732,000 katika wiki yake ya kwanza kwenye soko la Marekani.

Bifu kati ya Kanye West na Drake lilianza kuonekana wazi baada ya Drake kumchana Kanye kwenye ‘Duppy’ iliyokuwa imelenga kumshambulia Pusha T.

Inaelezwa kuwa huenda Kanye West ndiye aliyempa Pusha T siri za Drake ikiwa ni pamoja na kuwa na mtoto ambaye hakutaka ajulikane. Hii  ni kutokana na ukaribu uliowahi kuwepo kati ya Kanye West na Drake.

Hata hivyo, mvumo wa bifu kati ya Drake na Kanye hauhusishi lebo za Good Music na Young Money, kwani Kanye West alionekana akiwa na Lil Wayne (Bosi wa Young Money) kwenye harusi ya 2 Chainz.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 21, 2018
Museveni asema Bobi Wine hakujeruhiwa, amnukuu Trump