Msanii wa Bongo Fleva nchini, Godfrey Tumaini, maarufu kwa jina la ‘Dudu baya’ amekanusha tuhuma zilizotolewa na Mange Kimambi kuwa kipindi cha nyuma alishawahi kuishi na shoga nyumba moja.

Amekanusha tuhuma hizo alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa tuhuma hizo si za kweli na zimelenga kumchafua kuhusu kampeni yake ya kuwataja mashoga.

Amesema kuwa yeye kuwa karibu na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (Mashoga) si ajabu kwani yeye ni msanii hivyo kila mtu hupenda kuwa karibu naye.

Aidha, ameongeza kuwa mwanadada huyo anayeishi Marekani amekuwa na tabia ya kutunga vitu ambavyo havina ukweli wowote.

“Konki Konki Konki, Oili chafu, Master, huyu Mange anatunga vitu vya uongo kuhusu mimi, hawezi kunichafua kwasababu mimi tayari ni oili chafu na hawezi kupata taarifa za picha chafu kuhusu mimi,”amesema Dudu baya

Wahuu afunguka kuhusu majuto baada ya kuingia kwenye muziki wa injili
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Novemba 7, 2018

Comments

comments