Imewekwa rasmi kuwa Septemba 1, mwaka huu msanii toka Tanzania Naseeb Adbul, maarufu kama Diamond Platinumz akiwa ameshirikishwa na msanii toka Nigeria, Patoranking wataachia ngoma yao mpya kali inayoenda kwa jina la ‘Love you die’.

Mapema jana wasanii hao wametupia kionjo cha wimbo huo mpya ‘Love you Die’.

Ambapo kupitia instagram ya Diamond Platinumz amepost kipande kifupi cha wimbo huo na kukisindikiza kwa maneno haya ” My people !!! My Nigga Patoranking Got Something Delicious For you Coming out this 1st Septemba”.

Akimaanisha Watu wangu, kijana wangu Patoranking amewaletea kitu kitamu, kitaletwa kwenu Septemba 1, akiwa amenishirikisha”.

Washikiliwa na Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi
Israel yaituhumu Iran, yaitaka iache mchezo mchafu