Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Septemba 29, 2016 amefanya ziara ya kukagua maeneo mbali mbali jijini Dar es salaam yatakayo pandwa miti siku Oktoba mosi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu.

Makonda ametoa onyo kali kwa watu ambao wamekuwa wakiharibu miundo mbinu ya barabara na jiji kwa ujumla. Aidha Makonda ameliagiza  Jeshi la Polisi kujipanga kukabiliana nao ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria

Makonda pia amepongeza vyombo vya habari na wadau mbalimbali kwa kuunga mkono kampeni ya upandaji miti maarufu kama ‘Mti wangu’. Bofya hapa kutazama video.

Video: Tumejipanga vizuri kuelekea kilele cha kampeni ya Mti wangu
Roman Abramovich Akutana Faragha Na Antonio Conte