Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich ameonyesha kuwa sambamba na meneja wa kikosi cha klabu hiyo Antonio Conte, licha ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa, wawili hao wameanza kukwaruzana.

Taarifa za awali zilieleza kwamba, Abramovic alionyesha kuchukizwa na matokeo ya kupoteza michezo miwili ya ligi kuu ya soka nchini England iliyochezwa jijini London dhidi ya Liverpool na kisha Arsenal ambapo The Blues walikubali kupoteza.

Gazeti la The Times limeibuka na taarifa tofauti ambazo zinakinzana na fununu zilizokua zikizungumzwa kuhusu wawili hao kwa kuripoti bado wana mahusiano mazuri ya kufanya kazi kwa pamoja.

Abramovic anadaiwa kukutana na Antonio Conte kwa zaidi ya mara tatu kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ndani ya juma hili na wamekubaliana baadhi ya mambo ambayo yatafanikisha harakati za kukiboresha kikosi cha Chelsea.

Sehemu ya makubaliano hayo inatajwa kuwa ni maboresho ya kikosi cha Chelsea ambayo huenda yakafanywa wakati wa majira ya baridi (Januari 2017) kwa kufanya usajili wa wachezaji ambao wapo kwenye rada za Conte.

Meneja huyo kutoka nchini Italia amepania kuboresha safu ya kiungo ambayo kwa sasa inaongozwa na N’Golo Kante ambaye ameonyesha kutomudu baadhi ya majukumu uwanjani.

Lingine ambalo linaongeza chachu ya kufanywa kwa usajili klabuni hapo ni kuheshimu nafasi ya Antonio Conte, baada ya mkurugenzi wa michezo wa Chelsea, Michael Emenalo kuchukua nafasi kubwa wakati wa usajili wa N’Golo Kante pamoja na Michy Batshuayi.

Video: Makonda afanya ziara ya kukagua maeneo yatakayo pandwa miti Oktoba mosi
Picha: Clinton alimuibia Trump kwenye mdahalo? Wajuzi wanasa ‘kitu’ kwenye koti lake