Baada ya Hillary Clinton kutangzwa kumbwaga kwa kishindo Donald Trump kwenye mdahalo wa kwanza wa wagombea hao wanaowania Urais wa Marekani, wadukuzi wa mambo wameibua mjadala mwingine kupitia mitandao kuwa huenda kuna udanganyifu ulifanyika.

Clinton alipata asilimia 62 dhidi ya Trump aliyepata asilimia 27.

Kupitia mitandao, kimesambazwa kipande cha video na picha inayoonesha Clinton akiwa na kifaa ndani ya koti lake jekundu, kifaa ambacho kinaonekana kuwa ni ‘earpiece’ ambacho kutumika kupokea mawasiliano kutoka nje.

clinton-2

Kutokana na hayo, baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza kwenye mitandao ya kijamii kuwa huenda alikuwa anapata msaada wa maneno ya kusema kutoka kwa timu ya watu wake wakati mjadala unaendelea. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wanauliza kwanini alivaa kifaa hicho wakati Trump hakuwa na kifaa kama hicho. Je, ushindi wake ulichangiwa na udanganyifu?

Mtandao wa ‘Mirror’ umenukuu maswali yaliyoulizwa na mtandao wa Kikatoliki ulioweka picha ya Clinton akiwa na kifaa hicho, “Hiki kilikuwa kwa ajili ya nini?” Je, ni kifaa cha kuisaidia timu yake kumlisha majibu? Au ni kifaa maalum cha kudhibiti ugonjwa wa kifafa? Au ni kifaa cha kumsaidia kusikia?”

hillary-clinton-3

Muda mfupi baada ya kumalizika kwa mdahalo huo, Trump alilalamika kuwa kikuza sauti chake kilihujumiwa na kwamba hakikuwa kikitoa sauti kama ilivyokuwa inatakiwa.

“[Kikuza sauti change] kilikuwa kiko chini zaidi ya chake na kilikuwa kinakwaruza,” alisema Trump ambaye hata hivyo hakueleza ni namna gani hilo lilimpunguzia uwezo wa kujieleza.

Akijibu tuhuma hizo wakati alipokuwa kwenye ndege yake na  baadhi ya waandishi wake, Bi. Clinton alisema, “yeyote anayelalamikia kikuza sauti atakuwa hana usiku mzuri leo.”

 

Roman Abramovich Akutana Faragha Na Antonio Conte
Video: Mama alia kudhulumiwa nyumba 5, Aomba Rais Magufuli kumsaidia