Kupitia #SAUTIZETU ya dar24.co Mama mmoja mkazi wa Dar es salaam, Mushi Ernest amesema amedhulumiwa na ndugu yake nyumba tano huku Mahakama ikichangia kumkosesha haki zake pale kesi ilipofikishwa Mahakamani.

Mama huyo akiwa pamoja na nyaraka zake, katika harakati za kudai haki zake alimfuata Rais Magufuli katika Uwanja wa ndege wa Dar es saam Septemba 28, 2016 siku ya uzinduzi wa ndege mpya za Air Tanzania ili kumfikishia kero yake hiyo.

Mama Mushi alishindwa kuonana na Rais Magufuli lakini kupitia dar24.com ameeleza kilio chake akiomba msaada kutoka kwa Rais ili aweze kupata haki yake aliyodhurumiwa na ndugu yake ambaye ameshafariki dunia na kuacha mali hizo zikiendelea kuliwa na watu wengine hali yeye maisha yake magumu.

Picha: Clinton alimuibia Trump kwenye mdahalo? Wajuzi wanasa ‘kitu’ kwenye koti lake
Mo Dewji Aendeleza Neema Msimbazi