Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameagiza kubomolewa kwa Baa na Gesti zote zilizopo jirani na shule jijini Dar es salaam.

Makonda amesema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na maafisa elimu na waalimu wakuu, ambapo ameeleza kuwa ili wanafunzi waweze kusoma vizuri ni lazima kuondolewa kwa kelele zinazozunguka katika maeneo ya shule.

Pia, Makonda amewataka Waalimu Wakuu na Maafisa Elimu kukaa na kutoa tathmini ya shule ambazo zinahitaji ukarabati ili ziweze kukarabatiwa. ‘’Natoa siku ishirini kwa bar na gesti zinazozunguka maeneo ya shule zibomolewe kabisa kwani maeneo hayo si ya kufanyia biashara,”amesema Makonda.

Magazeti ya Tanzania leo Julai27, 2017
Majaliwa atoa agizo TCU, NACTE