Serikali imesema kuwa iko tayari kufanya kazi na makampuni ya matangazo ya biashara nchini endapo yataunda umoja na ushirikiano.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama katika uzinduzi wa  ushirika wa makampuni ya biashara.

“Mara nyingi tumeshindwa kutumia fursa nyingi zilizopo kwa ajili tu ya kukosa mshikamano, lakini kwa hiki mlichokifanya kwasasa mtapiga hatua kubwa,”amesema Mhagama

Hata hivyo, ameongeza kuwa hapo awali hapakuwa na mshikamano baina ya makampuni yanayofanya biashara, hivyo kupelekea makampuni hayo kukosa fursa nyingi.

Waziri ajiuzulu na kuhama chama tawala
Idadi ya waliokufa tetemeko Indonesia yazidi 800