Msanii chini ya Lebo ya WCB, Harmonize ameachia wimbo wake mwingine ambao kwa sasa unafanya vizuri katika chaneli za YouTube kwa kushika namba tatu kati ya video bora na kutazamwa zaidi katika mtandao huo.

Wimbo huo unaoenda kwa jina la ”Atarudi” akiwa amefanya video yake nchini Nigeria huko Lagos na Afrika Kusini.

Aidha mashabiki wake mbalimbali wametoa komenti zao juu ya ujio wa wimbo huo na kusema wimbo ni mkali na huenda Harmonize akawa mwanamuziki bora mwaka huu na kumpiku bosi wake Diamond Platinumz ambaye naye bado anafanya vizuri na nyimbo wimbo wa jibebe aliyoufanya na wasanii wake Lavalava na Mbosso.

Tazama video ya wimbo huo hapa chini kisha shusha komenti yako.

Makala: Kwa mwendo huu, Rich Mavoko ‘kazi anayo’ (Video)
Video: Dereva Bodaboda na Misukosuko Wanayopitia, "Nilitekwa nikatupwa Kinyerezi"