Q Boy Msafi ambaye amewahi kufanya kazi na lebo ya WCB ya Diamond Platinumz, ameeleza kufuta tofauti zilizosababisha kuachana na lebo hiyo.

WCB ndio lebo ambayo ilimtambulisha rasmi kwenye orodha ya mkondo A wa kiwanda cha burudani nchini akiwa kama mtaalam wa mavazi, akiwapanga kimavazi wanafamilia wa kundi hilo.

Akifunguka kupitia ‘The Plug’ ya Dar24, alipokuwa akipata chakula cha mchana kwenye ‘Real Burger’ iliyopo Bamaga jijini Dar es Salaam, Q-Boy alisema kuwa anayakumbuka mema 99 ambayo yanafuta kosa moja alilofanyiwa WCB.

“Watu wengi wanashindwa kuelewa… mtu anaweza kukufanyia kosa moja lakini akakufanyia mema 99, huyo hatakiwi kuwa adui,’ alisema.

“Huyo mtu hatakiwi kuwa adui kwa sababu kosa lake halijafuta mema 99. Kwahiyo ni mwanadamu na amekosa kama binadamu,” aliongeza.

Mkali huyo wa ngoma za ‘Mugacherere’, ‘Karorero’, ‘Unaanzaje’, na sasa ‘Wamevaa?’, amefunguka anachoki-miss hivi sasa kutoka kwenye lebo ya WCB pamoja na wanafamilia yake.

Angalia video hii kupata yote, anachoweza kuwasiliana na Zari na mengine:

TANZIA: Mwandishi wa habari afariki dunia
Askari mwenye bunduki ndani ya chumba cha mtihani azua gumzo