Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), Joseph Kabila Kabange amewasili nchini Tanzania jana October 03 2016 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Kabila amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na baadaye kushuhudia burudani ya vikundi vya ngoma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo leo October 04 2016 atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, ataweka jiwe la msingi la jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na baadaye kushiriki dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Tazama video ya Rais wa Congo DRC Joseph Kabila akiwasili nchini Tanzania tayari kwa ziara ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli

Modric, Lovren, Rakitic Kuzikosa Kosovo, Finland
ATCL yagusia Ratiba ya safari za ndege mpya, abiria walia na pengo la Fastjet