Mkali wa ‘Na Yule’, Ruby amerudi kwa njia ya aina yake  katika muziki baada ya ukimya wa muda mrefu kwa kumtambulisha mpenzi wake mpya ambaye kwa mujibu wake ni baba mtoto wake mtarajiwa.

Akizungumza hivi karibuni na Burudani24 ya Dar24, Ruby alieleza kuyafurahia mahusiano yake mapya na mpenzi ambaye alikuwa mpiga picha asiyefahamika kwa wengi.

“Nafurahia mahusiano yangu mapya na hakuna kitu ambacho nakikumbuka katika mahusiano yangu yaliyopita pia mashabiki wangu wakae tayari kwa ujio kazi mpya ambayo natarajia kuitoa hivi karibuni,” aliiambia Dar24.

Katika hatua nyingine, Ruby alifunguka kuhusu mtazamo wake kwa muimbaji mwenzake, Nandy ambaye baadhi ya watu wamekuwa wakidai amechukua nafasi yake. Mwimbaji huyo alieleza kuwa yeye pia ni shabiki wa Nandy na kwamba alianza kuwa shabiki wake tangu alipokuwa THT.

Ruby ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu akishiriki kwenye baadhi ya remix za nyimbo za wasanii wenzake kama ‘Sisikii’ ya Jux.

Odinga aapa kuweka mambo hadharani
Mpina kukabiliana na changamoto za muungano