Mashabiki wa msanii wa bongo Fleva, Janjaroo maarufu kama Dogo Janja wamekuwa na mapokeo tofauti kufuatia kibao chake kipya cha wimbo wa Wayu wayu alichomuimbia mke wake Irene Uwoya, ambapo mapovu mbalimbali yamewatoka mashabiki waliotazama video ya ngoma hiyo mara tu baada ya kuachiwa.

Video hiyo imeibua hisia za mashabiki kutokana na ubunifu uliotumika katika ngoma hiyo kwani dogo janja ameonekana kwa namna mbili tofauti, ya kwanza ikiwa ni sura yake kama mwanaume, ya pili ikiwa ni sura yake na matendo yake kama mwanamke.

Kufuatia sura hiyo ya pili aliyoicheza Dogo janja yakuigiza kama mwanamke imebua mapovu mengi kwa mashabiki na kuonekana kumpotezea alama za kufanya vizuri katika ngoma hiyo.

Kupitia mtandao wa kijamii wa instagram watu mbalimbali wametoa maoni yao wakiponda na wengine wakisifia namna tofauti ya ujio wa ngoma hiyo.

Baadhi ya maoni ya mashabiki yanasema

@Shafikihajiofficial ”Chali usikanyage Chuga tutakutoa pumzi”

@abdulaziz3538 ”kuanzia leo mi sio shabiki wake tena nahamia kwa msanii anayejielewa young killer”

@joycesamusoni ”Sema amesahau kunyoa ndevu”

Huku mashabiki wengine wakionekana kufurahia ubunifu huo na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya

@bahat_jonas   ”Watu wanaotoaa povu ni wajngaa hiyo ni sanaa bhana afu ni ubinifu toshaa saa nyiee kila siku mnatakaa kitu kile kile blaa kuchange bg up janjaro kazi nzuri”

@patrickjohnpj0069243   ”Big up sana ni ubunifu wa hali juu”

Mtandaoni kumepamba moto, pamoja na hayo yote nakubali kila mtu na mtazamo wake ndio maana kuna walioipokea vizuri kazi hiyo na walioipokea tofauti kazi hiyo.

Hongera Dogo janja kwa kazi nzuri, watanzania inabidi waipokee kama ilivyo kazi yako na waelewe ubunifu na uwezo mkubwa uliouonesha kwani si kila mtu anaweza kuwa na kipaji kama ulichojaaliwa nacho wewe, endelea kutuletea mambo mazuri.

Tupo pamoja kusapoti kazi za ndani, kutazama ngoma hiyo bonyeza linki hapo chini.

China yaondoa rasmi kwenye katiba ukomo wa urais
Rais Xi Jinping wa China kutawala maisha

Comments

comments