Klabu ya wana Jangwani, Young African ambayo hivi karibuni iliachana rasmi na mchezaji kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima imemulika suala la kuachana na mchezaji huyo na mpango wa kuliziba pengo lake.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Dar24, Kaimu Afisa Habari wa Mabingwa hao wa Tanzania Bara, Godlisten Anderson Chicharito amesema kuwa ingawa mchezaji huyo alikuwa na mchango mkubwa hakuwa na budi kuondoka kwani kadiri umri wake ulivyozidi kuongozeka ndivyo kipaji chake pia kilikuwa kikififia.

“Yanga wataangalia mchezaji mwingine anayefaa na watamtumia acheze nafasi yake. Kwa sababu hauwezi kumtumia mchezaji huyohuyo kwa miaka kumi au ishirini kwa sababu anazeeka na pia kipaji chake kinaenda. Kwahiyo lazima uangalie vipaji vingine,” Chicharito aliiambia Dar24.

Hata hivyo, alisema kuwa mchezaji huyo amekuwa na mchango mkubwa kwa klabu hiyo kwa muda wote wa miaka sita alioitumikia na kwamba ataendelea kuheshimiwa.

Katika hatua nyingine, Chicharito alizungumzia suala la upungufu wa washambuliaji wenye uwezo wa kupachika mabao nchini, hali inayowasukuma kusaka vipaji hivyo nje ya mipaka.

Angalia video hii kupata maelezo ya kina kuhusu mpango wa Yanga walichopanga kuifanyia Simba na klabu nyingine katika msimu ujao wa Ligi, mpango wa kumiliki uwanja wao binafsi kama timu ya kimataifa, mtazamo wake endapo Simba wangepewa ‘point’ za mezani kufuatia rufaa yao ili kushinda kombe la Ligi Kuu msimu uliopita na mengine mengi. Subscribe kupata habari punde tu zinapowekwa.

Maalim Seif aitaka jumuiya ya kimataifa kuiwekea vikwazo Tanzania
Video: Magufuli, Kikwete wazidiana kete, Kigogo Acacia anaswa 'kininja' Airport