Waanzilishi wa mtandao wa Instagram, Kevin York Systrom na Mike Krieger wametangaza wiki chache zijazo watajiondoa kabisa kujishughulisha na kampuni hiyo na kubaki kama watumiaji wengine wa kawaida mara baada ya mmiliki wa Facebook  Mark Zuckerberg kununua mtandao huo kwa dola za kimarekani $1 bilioni.

Kevin York Systrom ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu na Mike Krieger, Mkuu wa Ufundi wametangaza uamuzi huo ikiwa ni miaka sita baada ya kuiuza  na kwamba watabakia kama watumiaji wengine wa kawaida.

Mara baada ya mtandao huo kuuzwa umeendelea kufanya vizuri na mpaka sasa unawatumiaji zaidi ya bilioni 1 na kwa kipindi chote hicho waanzalishi wa mtandao huo wamekuwa wakifanya kazi katika mtandao huo wakiwa chini ya Mark Zuckerberg.

Taarifa hiyo ya kujiondoa imetolewa rasmi na mmoja ya waanzilishi wa Instagram Kevin York Systrom kupitia mtandao wake wa Instagram ambapo amesema.

”Tunahitaji kuchukua muda mwingi kuchunguza udadisi wetu na ubunifu wetu, kujenga mambo mapya inahitaji sisi kurudi nyuma na kuelewa nini kinatuhamasisha na pia kitu hiko kiendane na mahitaji ya dunia ndio tunachotaka kufanya” amesema Systrom

Katika taarifa yao ya pamoja wamesema wanajipanga kufanya udadisi upya katika masuala ya Mitandao ya Kijamii wamesema walipoanza mtandao huo wa Instagram umekua kutoka watumiaji 13 mpaka mamilioni ya watumiaji duniani kote kwa sasa.

 

Utafiti: Upweke kuwaumiza mamilioni zaidi
Bassogog arudishwa kikosini, Moukandjo akerwa na kustaafu

Comments

comments