Wabunge wa Jubilee nchini Kenya wamemtaka Jaji Mkuu wa Mahakama ya nchi hiyo, David Maranga kung’oka katika nafasi hiyo ikiwa ni siku chache baada ya kutengua matokeo ya uchaguzi mkuu uliompa ushindi, Uhuru Kenyatta.

Mbunge wa Nyeri Mjini kwa kupitia tiketi ya Jubilee, Ngunjiri Wambugu amefungua mashtaka katika tume ya majaji akitaka jaji huyo ang’olewe kwa kile alichokiita utendaji wake mbaya hivyo hastahili kuendelea na kukalia nafasi hiyo.

Aidha, Mbunge huyo ambaye amewasilisha mashtaka yenye kurasa 14 ameomba tume ya majaji kwa kushirikiana na mahakimu kuanzisha uchunguzi dhidi ya jaji maranga ili kubaini mwenendo wake tangu kuteuliwa katika nafasi hiyo.

Wanamgambo 6 wa Al-Shabaab wauawa

Mugabe amzuia msanii wa kike kuingia Zimbabwe kwa kutovaa nguo za ndani

Hata hivyo, Wambugu amedai kuwa Jaji maranga ametekwa na mashirika ya kiraia ambayo yamekuwa yakiupinga utawala wa rais Uhuru Kenyatta tangu mwaka 2013.

 

Argentina yahamia Estadio Alberto J. Armando (La Bombonera)
Wanawake jinsi ya kuutambua ugonjwa wa 'Fibroids'