Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu  hapa nchini wameshauliwa kutumia muda wao kujisomea na kuepuka kujiingiza kwenye vitendo vya vurugu , migomo na maandamano yasiyo na tija kwa taifa.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi  Kinondoni, Suzan Kaganda alipokuwa akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kwenye kongamano la 3 lililowakutanisha wahitimu wa chuo hicho.

“Naomba nisisitize kuwa elimu mliyoipata na mnayoendelea kuipata chuoni hapa sio kwa ajili ya manufaa yenu binafsi bali ni kwa ajili ya manufaa ya taifa, wakati mwingine mnapoteza muda mwingi kujiingiza kwenye migomo na maandamano barabarani kushindana na Serikali, muda ambao mngeutumia kujisomea ninyi  wenyewe”  Amesema Kamanda Suzan.

Aidha, amekipongeza chuo cha CBE kwa kupiga hatua na kupata mafanikio makubwa katika utoaji wa elimu tangu kuanzishwa kwake miaka 51 iliyopita kwa kuwa maendeleo makubwa kwani taifa lolote haliwezi kupata maendeleo bila kuwaelimisha watu wake katika biashara na Ujasiriamali elimu inayotafsiri uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha CBE, Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa kongamano hilo amesema kuwa chuo anachokiongoza kimeendelea kupata sifa ya kuwa chuo bora ndani na nje ya nchi kwa kuwa kimetoa viongozi mahiri ambao wametoa  mchango katika maendeleo ya taifa

 

 

 

 

Video: Zitto agusa hisia za wabunge akiaga mwili wa Sitta
Janeth Magufuli aruhusiwa kutoka hospitalini