Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Emmanuel Songoye ameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi  katika kijiji cha kabanga wilayani Kasulu mkoani Kigoma kwa tuhuma za kudaiwa kuwa mshirikina.

Kufuatiwa na tukio hilo pia wananchi wa kijiji hiko wameteketeza kwa moto nyumba saba, magari mawili, pikipiki nne, na mali za familia za watu sita ambao wanatuhumiwa kufanya mauaji ya watu kijini hapo kwa njia mbalimbali ikiwa pamoja na ushirikina ili watajirike.

kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Naibu kamishna wa polisi Ferdinand Mtui amesema zaidi ya watu hamsini wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo kwa kijichukulia sheria mkononi.

Aidha kaimu mkuu wa wilaya ya Kisulu Kanali Marco Gaguti ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuiachia serikali kushughulikia matokio hayo.

 

Breaking: Miili ya watoto wawili yaopolewa shimoni Arusha
Video: Christian Bella sasa atamba na 'Punguza kidogo'