Wasanii wa muziki nchini Marekani Justin Beiber na Dj Khaled wameonekana wa kipekee nchini kwao kutokana  ushirikiano mkubwa wanaouonesha katika jamii zinazowazunguka.

Hivyo wasanii bongo wachukue hii kutoka kwa Justin Beiber na Dj Khalid, kurudisha fadhila katika jamii hasa kwa wale wahitaji wasio na uwezo na sio kuhonga na kupotosha mabinti kuwa laghai na kuwapa mimba.

Msanii Justin Beiber jana amefanya ziara ya kushitukiza katika moja ya hospitali ya kuhudumia watoto huko nchini kwao na kuwafariji watoto wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali kwa kula kucheza, kuimba na kusali pamoja nao.

Watoto hao wamesema wamesikia faraja kubwa kwani walipata nafasi ya kupiga picha na msanii huyo mkubwa nchini ambapo kutokana na matatizo yao ya kiafya hawakuwahi kufikiria kuja kuonana nae.

Mbali na msanii huyo Dj Khaled pia ni msanii maarufu nchini marekani anayefanya vizuri katika kazi zake za sanaa ya muziki.

Siku chache zilizopita nyimbo zake zimekuwa zikifanya vizuri katika chat ya nyimbo za Billboard na kushika nafasi ya kwanza mfulululizo kwa muda wa wiki mbili.

Kama namna ya kujipongeza msanii huyo ambaye anamiliki kiwanda cha nguo nchini humo aliamua kufurahia kazi yake ya muziki kwa kusaidia idadi kubwa ya wanafanzi nchini kwao kwa kuwashonea sare za shule wanafunzi wote ambao walikua hawana uwezo wa kufanya hivyo.

Dj khalid alisambaza sare hizo kama ishara ya kufurahi na kujipongeza kwa kile anachokifanya katika muziki wake.

 

 

Samia Suluhu azindua huduma mpya ya fedha ya TTCL PESA
Video: Jerry Muro atema 'cheche' aiponda kamati ya maadili ya TFF iliyomhukumu