Tamasha  la kwanza la Muziki la Serengeti linafanyika  leo katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumzia tamasha hilo Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.  Hassan Abbasi amesema  tamasha hilo ni maalaum kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa karibu kwa sekta za sanaa na utalii nakutoa shukrani kwa wasanii

Dkt Abbas amesema kuwa maandalizi yamekamilikana na kuwataka watanzania kufika kwa wingi kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

“Maandalizi ya tamasha yamekamilika, wana Dar es Salaam na mikoa ya jirani nawakaribisha wajekupata burudani kutoka kwa wasanii wao. Kutakuwepo na burudani za kila aina na ulinzi ni wauhakika,” amesema Dkt Abbasi

Pia amesema tamasha hilo la bure ni maalumu kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wasanii wa zamani kutokana na mchango wao wa kusaidia kukua kwa tasnia ya muziki nchini na kufanya ionekane kama chanzo cha mapato ya mtu mmoja mmoja na taifa na siyo uhuni.

Aidha, Dkt Abbasi amesema kesho kutwa kutakuwa na mwendelezo wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni litakalofanyika Bagamoyo katika chuo cha TaSUBa na kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwamo ngoma za asili.

Ujerumani kuanza kutoa chanjo ya Corona
Majibu ya Covid- 19 kutolewa ndani ya saa 24