Mtu mmoja, Mfanyabishara Hery Sengo (44), mkazi wa mtaa wa Msimamo kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro ameuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na watu ambao bado hawajafahamika.

Akizungumza na Dar24, shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mke wa marehemu aitwaye Saileni, amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa nane usiku wakati wakiwa wamelala na walivamiwa na watu watatu ambao walikuwa wameficha sura zao.

Amesema, watu hao walifika nyumbani kwao kisha kuvunja mlango wa nyuma nakuingia ndani na kumtaka mumewe aoneshe suruali aliyovaa mchana na katika mabishano ndipo wakamchoma kisu shingoni na akapoteza maisha.

Waombolezaji wakiwafariji wafiwa msibani Kihonda Morogoro.

Mara baada ya tukio hilo, Mwanamke huyo (Saileni), akikimbia nje na kupinga kelele ili kuomba msaada na amesema hata hivyo watu hao hawakuchukua kiasi chochote cha fedha ila waliondoka mara baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Mwenyetiki wa mtaa wa Msimamo uliopo kata ya Kihonda, John Mazimba amesema kwa sasa wameanzisha mpango wa ulinzi shirikishi, ili kudhibiti matukio ya uhalifu katika mtaa huo, huku Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, SACP. Fortunatus Musilimu akithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kocha wa viungo kutangazwa Simba SC
Polisi wajipanga kung'oa mizizi ya uhalifu