Waziri mkuu mteule wa Lebanon, Mustapha Idib leo ameazisha mazungumzo ya kuunda serikali itakayoshughulikia utatuzi wa mgogoro, chini ya shinikizo la Ufaransa kuhitimisha jukumu hilo ndani ya wiki mbili.

Mashauriano hayo yanafuatia ziara ya ngazi ya juu kabisa ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambapo katika safari hiyo alisema viongozi wa kisiasa wamekubali muongozo wa kisiasa kwa ajili ya mabadiliko.

Adib ameanza kukutana na viongozi wa bunge kipindi hiki kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis akionya kwamba Lebanon inakabiliwa na hatari ambayo inatishia hata uwepo wa taifa hilo na kwamba taifa hilo haliwezi kuachwa peke yake.

Mabadiliko hayo yanakuja kufuatia mlipuko mbaya wa mwezi uliopita katika bandari ya Beirut.

kwanini utumie tangawizi
Platini kitanzini tena