Jeshi la Polis Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuwa litaanza mara moja utekelezaji wa sheria ya kuwakamata wale wote walioweka stika za giza katika vioo vya magari yao, maarufu kwa jina la ‘tinted’.

Msako wa kuyamata magari yote yaliyowekwa vioo vya tinted za mtaani , umeatangazwa kuanza kesho huku watumiaji wakitahadharishwa kuondoa mara moja kwani sheria itawashughulikia ipasavyo.

Aidha, agizo hilo limeibua maswali mengi kwa wananchi na watumiaji wa magari hayo dhidi ya utata wa amri hiyo kuwa ni sheria au kanuni ipi iliyotumika kupiga marufuku na kamata kamata hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya wadadisi wanahoji kuwa ni kifaa kipi ambacho kitatumika kutofautisha kati ya tinted za mitaani na zile ambazo zinahitajika kwa matumizi katika magari , ambazo ni sahihi.

Video: walioshindwa kuendeleza viwanda wanyang'anywe-JPM
?LIVE: Rais Magufuli akihutubia wananchi katika uzinduzi wa kiwanda cha saruji Tanga