Watu watano wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha gari ndogo, ya Wizara ya Kilimo na Chakula na lori iliyotokea eneo la Njirii Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

Taarifa za awali zinadai kwamba gari dogo lilikuwa limebeba wataalamu wanne pamoja na dereva, wote wamefariki papo hapo ambapo wanaume walikuwa watatu na wanawake wawili.

Akithibithisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amesema kuwa miili imehifadhiwa ktk Hosptali ya Wilaya Manyoni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ametaarifu kuwa Wizara ya Kilimo imepatwa na msiba wa Watumishi wake Watano (5) waliopata ajali Manyoni mkoani Singida, walipokuwa safarini kuelekea Mwanza kikazi. Watumishi hao waliofariki ni;
1. Stella Joram Ossano (39)
2. Esta Tadayo Mutatembwa (36)
3. Abdallah Selemani Mushumbusi (53)
4. Charles Josephat Somi
5. Erasto Mhina (43)

China, Tanzania bega kwa bega sekta ya uwekezaji
Video: Tazama ngoma mpya ya Professor J na Harmonize 'Yatapita'

Comments

comments