Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga SC wameanza vyema katika kampeni za kuwania kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa baada ya kuwachapa mabao 4-0 wenyeji Zalan FC kutoka nchini Sudan Kusini mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga SC walipata mabao ya yote manne kipindi cha pili mara baada ya kipindi cha kwanza timu zote kwenda mapumziko bila kufungana.

Mshambuliaji hatari kwa sasa Fiston Mayele amefunga hat-trick akifunga dakika 45,85 na 88 huku bao moja likifungwa na Fei Toto dakika ya 55.

Yanga SC watarudiana na Zalan FC Septemba 16,2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwa kama wenyeji.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 11, 2022
Simba SC yakiwasha ugenini