Mabingwa wa soka Tanzania Bara Young Africans leo wameanza kampeni ya kuusaka ubingwa wa Afrika kupitia michuano ya ligi ya mabingwa barani humo, kwa kucheza mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali dhidi ya mabingwa kutoka Shelisheli St Louis.

Young Africans wamecheza mchezo huo wakiwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri, lililofungwa na Juma Mahadhi katika dakika ya 67.

Hata hivyo katika dakika ya 27, Young Africans walikosa nafasi ya kuongoza bao, kufuatia mshambuliaji wao Obrey Chirwa kukosa mkwaju wa penati uliotokana nay eye mwenyewe kuangushwa katika eneo la hatari.

Ushindi huo unaiweka Young Africans katika mazingira ya ushindani zaidi pindi itakapokwenda ugenini visiwani Shelisheli majuma mawili yajayo.

Kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa alizungumjza na waandishi wa habari mara baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, na kuesema kikosi chake kilicheza vizuri na kimefikia lengo la kushinda katika uwanja wa nyumbani.

Simba kuikabili Gendamarie kesho
Makonda kupitia upya taaluma za wanasheria, asimamisha kesi zote

Comments

comments