Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara  Young Africans kitaondoka jijini Dar es salaam leo jioni kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho (Azam Sport Confedaration Cup).

Msafara wa wachezaji, benchi la ufundi na viongozi utaondoka saa 11 jioni na ndege ya shirika la ndege la ATC.

Wachezaji watakao ondoka ni Makipa: Deogratius Munishi ,Beno Kakolanya na Ally Mustapha. Nafasi ya ulinzi ni Nadir Haroub,Vicent Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani.

Nafasi ya viungo ni Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke,Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimoni Msuva, Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin.

Upande wa washambuliaji ni Amissi Tambwe , Matheo Antony na Obrey Chirwa.

Wachezaji watakaoukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali ni  Malimi Busungu, Vincent Bossou na Donald  Ngoma.

Salum Mkemi Kufuata Nyayo Za Haji Manara
Rais Museven akosolewa vikali na wabunge