Msanii anayefanya vizuri katika muziki wa rap na sasa anatamba na ngoma yake aliyomshirikisha Harmonize kutoka lebo ya WCB ‘Unaionaje’ , Yaungkiller Msodoki  amefunguka kuhusu  maneno yanayovuma chini ya kapeti  kuwa yupo mbioni kufanya kazi zake chini ya usimamizi wa lebo ya WCB, Wasafi.

Youngkiller, amekanusha tetesi hizo na kusema kuwa yeye na lebo ya WCB kinachowaweka pamoja ni biashara na kazi, na sio kufanya kazi chini ya mkataba kama msanii wa lebo hiyo kama inavyodhaniwa na wengi.

“mimi siko Wasafi lakini nafanya nao kazi kama ambavyo watu wanaweza kutazama na mnavyoona” Amesema Youngkiller .

Hata hivyo Youngkiller amesema kuwa video ya ngoma hiyo ni moja ya video zake kali ambazo ameamini kuwa haitakuwa rahisi kuvunja record ya uzuri wa video hiyo iliyoshootiwa Afrika ya Kusini na muongozaji Nic.

Tazama video yake hapa chini.

China yaikingia kifua Korea Kaskazini dhidi ya 'makombora' ya Marekani
JPM afanya uteuzi mwingine