Msanii Z-Anto amefunguka mipango yake mikubwa ya kurudi kwenye kiwanda cha burudani ambapo kwa muda mrefu amekua kimya akidai ni kutokana na changamoto mbalimbali alizozipitia.

Z-Anto katika mahojiano na Dar24 Media kaitika usiku wa Mashindano ya ulimbwende yaliyohusisha Viziwi, amesema Ngoma yake ya Binti Kiziwi ndio iliyomfanya kuitwa katika tukio hilo na amechukua kama Heshima kubwa kwa kuwa ni wimbo wa zamani ila unakumbukwa kwa umuhimu wake.

Msanii huyo ambae alikua pamoja na aliekua mke wake ambae aliimba nae wimbo wa Binti Kiziwi kwa pamoja wamesema kwa sasa hawana mahusiano ya kimapenzi isipokua ni heshima ya kazi na familia kwa sababu walikua na ukaribu kwa familia zote mbili.

Waili hao wamedai kwa wakati huo walikurupuka kufanya ndoa kutokana na utoto.

Je Unafahamu sababu za Vijana wengi kunywa Pombe kali kupindukia?
Agizo la Rais Samia tozo za mafuta