Zaidi ya wafanyabiashara 1000 halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani humo wanatarajia kupata fursa ya vibanda katika Soko jipya na la kisasa linalojengwa mjini Njombe.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Edwirn Mwanzinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa soko hilo litakuwa na ghorofa moja, linaweza kuchukuwa miezi nane kukamilika kutokana na mda aliopewa mkandarasi wa soko hilo huku gharama ya ujenzi huo ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni 9 ikiwa ni fedha za mkopo kutoka benki ya dunia.

“Huu mradi tumeanza nao mwezi wa kumi na mbili ambao inatakiwa uchukuwe miezi nane kukamilika kama mkataba unavyosema lakini inawezekana tusifaulu kwa miezi hiyo kwakuwa wakati tunaanza tayari tulikuwa tunaingia katika kipindi cha kifuku, ila kwa kifupi tunakwenda vizuri kama mnavyoona mkandarasi yupo vizuri na amejipanga kazi inakwenda katika viwango licha ya kuwa na hii mvua”amesema Mwanzinga

Naye msemaji wa kampuni ya ujenzi ya Nandura gng & construction co.ltd Lalir Kumar Jangir amesema kuwa miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo ni pamoja na ugumu wa upatikanaji wa vifaa kama kokoto lakini haviwezi kupunguza kasi yao ya ujenzi.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara, Geophrey Anton na Scola kyando wamesema kuwa kukamilika kwa soko hilo kutawasadia kupunguza gharama ya kupata fremu nje ya soko,na kupata wateja tofauti na ilivyo sasa kutokana na umbali wa soko lillipo kwa kuwa wateja imekuwa ni ngumu kufika.

Kukamilika kwa soko hilo kutasaidia kuongezeka kwa pato la halmashauri ya mji huo kutokana na uwingi wa wafanyabiashara watakaoingia katika soko hilo.

Ajali mbaya yatokea mkoani Songwe
DC Kasulu akemea vitendo vya ukatili kwa watoto