Wizara ya Afya nchini Malawi, imesema Ugonjwa wa kipindupindu, ulioripotiwa na unaoendelea tangu mwezi Machi 2022 katika Taifa hilo, umeuwa zaidi ya watu 1,000 huku ikisema ongezeko la vifo linatokana na ukosefu wa chanjo.

Shirika la Afya Duniani (WHO), limesema idadi ya vifo ilifikia 1,002 siku ya Jumanne Januari 23, 2023, na kufanya mlipuko wa sasa wa kipindupindu kuwa mbaya zaidi katika rekodi katika nchi hiyo ambayo hapo awali ilishuhudia vifo 968 miaka ya 2001 na 2002.

Muhudumu wa Afya akiwajibika. Picha ya Anadolu Agency.

Jumla ya watu 30,600 wameambukizwa maradhi hayo, tangu kesi za kwanza kuonekana mwaka jana na inaelimishwa kuwa Kipindupindu huambukizwa kwa kunywa maji au kula chakula kilichoambukizwa na bakteria. Kwa kawaida husababisha kuhara na kutapika na inaweza kuwa hatari sana kwa watoto wadogo.

Msemaji wa Wizara ya Afya, Adrian Chikumbe amesema hadi kufikia mwezi Novemba 2022, Malawi ilikuwa imepokea karibu dozi milioni tatu za chanjo ya kumeza kutoka kwa Umoja wa Mataifa, lakini ilitumia chanjo zote zilizokuwepo.

Teuzi na panga pangua ya Wakuu wa Wilaya, Shaka aibukia Kilosa
Bigirimana: Nimeondoka kwa salama na amani