Wakati msimu wa 2017/2018 ukitarajiwa kufikia kikomo Mei 31, 2018 kwa mujibu wa Kalenda ya Mashindano ya Shirikisho la soka nchini TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza timu zilizofanikiwa kupanda daraja kwa msimu ujao.

TPLB ambao ndiyo waendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) mbali na kutangaza timu hizo zilizopanda daraja, pia imetoa pongezi kwa viongozi, wachezaji na mashabiki waliowezesha mafanikio hayo kwa msimu wa 2017/18.

Kwa upande wa ligi daraja la kwanza (FDL) timu zilizothibitishwa na TPLB kupanda daraja na kucheza ligi kuu msimu ujao kulingana na msimamo wa mwisho wa Ligi hiyo ni,

Kundi A ni JKT Tanzania FC ya Dar es Salaam na African Lyon ya Dar es Salaam.

Kundi B ni Kinondoni Municipal Council FC ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga wakati Kundi C ni Biashara United FC ya Musoma na Alliance Schools FC ya Mwanza.

Kwa upande wa ligi daraja la pili (SDL) zilizopanda kwenda ligi daraja la kwanza (FDL) msimu wa 2018/2019 ni timu nne zilizoongoza makundi pamoja na washindwa bora (best looser) watatu. Kundi A ni Reha FC ya Dar es Salaam, Kundi B ni Arusha FC ya Arusha, Green Warriors ya Dar es Salaam, na Mashujaa FC ya Kigoma.

Washindwa bora ni Namungo FC ya Lindi,  Pepsi FC ya Dar es Salaam, na Boma FC ya Kyela, Mbeya.

Wallace Karia awaaga vijana wa TSC
Umoja wa Ulaya wapingana na Trump kuhusu Iran