Kufuatia uamuzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wa kuwafikisha Mahakamani wafanyabiashara wawili, James Rugemalira na Harbinde Seth ambao ni watuhumiwa wa kesi za ESCROW na IPTL, Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi huo.

Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma mjini amesema uamuzi huo ni hatua kubwa na yakupongezwa. “Rais magufuli nimekuwa nakupinga kwenye mambo mengi na nitaendelea kukupinga, lakini kwenye hili umeitendea haki nchi. Hongera sana”.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Watuhumiwa hao wamefikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu leo Juni 19, 2017 kwa makosa ya uhujumu uchumi ambapo baada ya hatua hiyo ya TAKUKURU, Zitto Kabwe ametoa maoni yake kupitia ukurasa wake wa tweeter.

Video: Uamuzi ya Mahakama kuhusu James Rugemalira na Harbinde Seth
Meya wa Ubungo ashikiliwa na Jeshi la polisi

Comments

comments