Kocha Mkuu wa Simba SC Zoran Maki amemkingia Kifua Mshambuliaji wake kutoka nchini Serbia Dejan Georgijevic ‘MZUNGU’, ambaye amekua gumzo kila kona ya nchi.

Dejan alisajiliwa Simba SC siku moja kabla ya Tamasha ya Simba Day na ameshacheza michezo miwili ya kiushindani (Ngao ya Jamii na Ligi Kuu) na mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya St George.

Kocha Zoran amesema anajua watu wengi wana kiu ya kutaka kuona makali ya Dejan, ila hana mashaka na Mshambuliaji huyo, kwani muda mfupi ujao wataona ubora wake.

Amesema Mshambuliaji huyo bado hajazoeana na wachezaji wenzake kutokana na kuchelewa kujiunga na timu, hivyo bado anatafuta muunganiko.

“Inahitaji muda kidogo, alichelewa kujiunga na timu, mnakumbuka alikuja wakati tunatoka Misri ni muhimu akazoeana na wenzake na wao wakajua ni mpira gani anahitaji,”

“Ni Mshambuliaji bora sina wasiwasi naye, ni vile wakati sio rafiki, anahitajika kupambana kuonyesha kile kitu halisi alichonacho.” amesema Kocha huyo kutoka Serbia

Katika hatua nyingine Kocha Zoran amesema kikosi chake kitacheza mchezo mmoja ama miwili ya Kirafiki, wakati ligi itakaposimama kupisha Michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Bingwa ya Afrika ‘CHAN’ na Fainali za Afrika ‘AFCON’.

Amesema michezo hiyo ya kirafiki itamsaidia Dejan kujipanga vyema kabla ya kurudi Uwanjani kufanya mambo yake kwenye michezo ya ushindani.

Urusi, Ukraine zashutumiana mapigano karibu na Nyuklia
RC Shigella aagiza mipango thabiti maeneo muhimu