Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu amevunja Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge, ambalo limemaliza kipindi chake cha miaka mitatu ya uhudumu.

Zungu amevunja Baraza hilo la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge katika kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Jijini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu wakati alipokuwa akitoa hotuba ya kuvunja Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Baraza hilo limemaliza kipindi chake cha miaka mitatu.
Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi akitoa hotuba ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Naibu Spika, Mussa Zungu kuvunja Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitatu.
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Bunge, Chacha Nyakega akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge.

Ajali nyingine ya Basi Mkoani Kilimanjaro
Ajali ya Basi yauwa 20, wamo watoto 11