Klabu ya Young Africans huenda ukaachana na wachezaji 14 mwishoni mwa msimu huu, huku ikitarajia kujaza nafasi zao wakati wa usajili kuelekea msimu mpya wa 2022/23.

Wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye mpango wa kuachwa klabuni hapo, ni wale ambao wameshindwa kufikia viwango vya Benchi la Ufundi la klabu hiyo chini ya Kocha Mkuu Mohamed Nabi, ambaye msimu huu anakaribia kurejesha heshima ya ubingwa.

Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye mpango wa kutemwa Young Africans ni David Bryson, amecheza michezo sita, Abdallah Shaibu (mchezo mmoja), Deus Kaseke (michezo kumi) na Heritier Makambo (michezo kumi na nane), Yusuph Athuman (michezo sita), Yassin Mustapha (michezo tisa), Paul Godfrey (mchezo mmoja), Crispin Ngushi (michezo mitatu), Dennis Nkane (michezo kumi), Balama Mapinduzi (mchezo mmoja), Chico Ushindi (michezo mitano) na Ibrahim Abdallah (michezo miwili).

Wengine ni Walinda Lango Erick Johore na Ramadhan Kabwili, ambao hawajacheza hata mchezo mmoja wa ligi msimu huu.

Tayari klabu hiyo imeshatangaza kuachana na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza, baada ya kumaliza mkataba wake, huku akihusishwa na utovu wa nidhamu wakati timu ilipoweka Kambi jijini Mwanza kwa maandalizi ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC”.

Manara afichua siri ya usajili Young Africans
Biashara United Mara yaomba msaada Ligi Kuu