Uwepo wa mila potofu katika jamii hasa ile ya wanaohama hama makazi umekuwa ukichangia uwepo wa changamoto ya watoto kutopatiwa chanjo, na kupelekea athari ya kiafya kwa watoto.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mpango wa Chanjo Taifa, Dkt. Florian Tinuga katika semina elekezi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo mikoa ya Kanda ya Kaskazini, na kusema elimu itasaidia uondoaji wa dhana hiyo kwa wazazi na walezi.
Amesema, “tunasimamia chanjo makundi manne, kundi la kwanza ni chanjo za watoto chini ya miaka mitano, na upande wa wanawake na wasichana wenye umri wa miaka 14 ila bado mwitiko ni mdogo hasa kwenye dozi ya pili.”
Hata hivyo, ameongeza kuwa suala la mila potofu halina uzito kwa kwa chanjo ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano bali kwa hutokea kwa wale wenye umri wa juu huku akisema chanjo inayoingizwa nchini haina tatizo.