Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha the Citizens Coalition for Change (CCC), Nelson Chamisa ametangaza kujiuzulu miezi michache baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa urais, akilaani vitisho na vurugu zinazofanywa watawala.

Chamisa amekishtumu chama tawala cha ZANU PF cha Rais Emmerson Mnangagwa kutumia vyombo vya dola kukidhoofisha chama cha CCC.

“Hii ni kuwatangazia rasmi raia wenzangu wa Zimbabwe na dunia nzima, kwamba kuanzia sasa, sina uhusiano wowote tena na chama cha CCC,” Chamisa amesema katika taarifa.

Uamuzi huo, unajiri baada ya Mnangangwa (81), kushinda muhula wa pili katika uchaguzi ambao ulikipa chama tawala cha ZANU-PF wingi wa viti katika bunge.

Simba SC yaanza kambi bila Benchikha
Simon Msuva afichua safari ya Saudia