Kiungo wa Manchester City anayecheza kwa mkopo West Ham, Kalvin Phillips amemchana kocha wake Pep Guardiola juu ya kauli yake ya kumwambia yeye ni mzito sana.

Guardiola alisema staa huyu wa kimataifa wa England hayupo sawa kwa ajili ya kufanya mazoezi na timu baada ya kurejea kwake kutoka Kombe la Dunia mwaka 2022.

Phillips amesema kauli hiyo ilikuwa ngumu sana kwake na familia yake iliona kauli hizo zilikuwa zimevuka mipaka.

Staa huyo alijiunga na West Ham kwa mkopo dirisha la majira ya baridi mwaka huu baada va kuona nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Man City ni ndogo.

Wakati Pep ametoka hadharani na kusema vile, alikuwa sahihi lakini alitakiwa atumie njia nyingine tofauti, sipingi alichosema lakini maneno yake yalishusha sana hali yangu ya kujiamini na jinsi nilivyokuwa najiona kwenye kikosi cha Man City, hata familia yangu haikufurahia jambo hili, sana sana mamna yangu.

Guardiola, ambaye pia aliwahi kumwacha Sergio Aguero kutokana na kuzidi uzito amekuwa akichunga sana suala hili kwa wachezaji wake.

Watu wanasema tu nilizidi uzito, lakini kuzidi uzito huwa ni kilo 10 baadhi ya watu lakini mimi nilizidi kilo 1.5 tu, nafikiri Pep alichukizwa na kitendo cha mimi kuchelewa kurudi mazoezini mapema na hiyo ilisababishwa na kutokuelewana kwenye mawasiliano baina yangu na wahusika wanaosimamia masuala hayo,” alisema Phillips ambaye alichelewa kujiunga na timu kwa siku 10 baada ya England kutolewa kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2022.

“Ndio kwanza nilikuwa nimetoka kupona bega langu na Pep alihitaji niwasili kambini siku moja baada ya kutoka kwenye kambi ya England ili niweze kucheza mechi za kirafiki, lakini mimi sikupewa taarifa hizi, kama ningeambiwa ningefanya hivyo.”

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 13, 2024
De Jong kucheza England 2024/25