Viwango vya Demokrasia Duniani kwa mwaka 2023 vimeripotiwa kuwa vilishuka kutokana na uwepo wa vita, ukandamizaji wa haki kimabavu na kupungua kwa uaminifu katika vyama vikuu vya kisiasa.

Hayo yamebainishwa na kitengo cha utafiti cha shirika la Economist ambacho kimesema ulimwengu umeingia katika enzi ya migogoro na mikondo ya vita kuu na hatua hiyo itatoa taswira za uwepo wa hatari katika siku zijazo na kwamba vita vya sasa vimejikita katika nchi ambazo demokrasia haipo au zipo katika matatizo.

Kitengo hicho cha utafiti kimedokeza uwepo wa ongezeko la upingaji wa wahamiaji katika nchi nyingi kwani hali ya kisiasa barani Amerika na Ulaya, imezidi kuwa na mgawanyiko.

Aidha, ripoti hiyo imebanisha kuwa, nchi za Norway, New Zealand na Iceland ziko nafasi ya juu katika demokrasia wakati Korea Kaskazini, Myanmar na Afghanistan zikishika mkia.

Mradi LTIP kuwanufaisha Wazawa upimaji, upangaji
Tanzania mwenyeji Kongamano la Petroli Afrika Mashariki