Jeshi la Israel – IDF, limewakamata watu 100 wanaoshukiwa kwa shughuli za ugaidi kwenye Hospitali ya Nasser iliyopo mji wa Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza.

IDF iliingia kwenye majengo ya Hospital hiyo kwa lengo la kukomboa miili ya mateka wa Israel, waliokuwa wakishiliwa na Hamas na ndipo lilifanikisha ukamataji huo.

Aidha, imesema linaendelea na operesheni yake ilioitaja sahihi na yenye mipaka dhidi ya kundi la Hamas ndani ya hospitali hiyo ilioko kusini mwa Gaza.

Hata hivyo, Wizara ya afya Gaza inayoongozwa na Hamas imesema wagonjwa wengi wakiwemo watoto wapo hatarini, huku ikishutumu Israel kwa kuzuia kuhamishwa kwa wagonjwa kwenda hospitali nyingine.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 19, 2024
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 18, 2024