Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa – LAAC, imeielekeza Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Kufanya ufuatiliaji na uchunguzi wa fedha walizopeleka kutekeleza miradi katika Mkoa wa Manyara, hasa katika miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamati katika muendelezo wa ziara ya kikazi katika mkoa wa Manyara kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na Babati ambapo Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ester Bulaya alieleza kutokufuraishwa na usimamizi, ufuatiliaji, ufanisi na ubora wa miradi, kutokukamilika kwa wakati katika mkoa huo.

Amesema, Serikali inatakiwa inatafuta fedha za uwekezaji wa miradi ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wananchi wa maeneo husika, lakini wapo baadhi ya watumishi wanakosa uadilifu na uaminifu na kufanya fedha hizo kama za bure ilihali zinatoka katika kodi za wananchi.

 

Ameitaja miradi ambayo bado haijakamilika kuwa ni pamoja na mradi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, ambao fedha zake zilishatolewa na bado Halmashauri imeomba kuongezewa fedha za kumaliza miradi hiyo.

Bulaya amesema tabia iliyozoeleka kwa baadhi ya Halmashauri zikipewa fedha za miradi na zikimaliza fedha hizo husema zitaomba Ofisi ya Rais TAMISEMI na zitaongezewa sio sawa, kwani inawalemeza na kuwataka kuangalia lengo la kuanzishwa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na wajue kuwa kwa vitu vidogo lazima wajitegemee.

DKT. Biteko ashiriki sherehe za kusimikwa Askofu mpya Mafinga
GGML yawapa mbinu Geita Boys kuyafikia malengo kitaaluma