Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani, kimeendelea na operesheni ya kutoa elimu na kuwakamata wale wanaoendelea kuvunja sheria za Barabarani na kuwapongeza wote waliotii agizo la Serikali la kuondoa namba ambazo hazijadhibitishwa na Shirika la – TBS.

Akiwa katika Operesheni hiyo leo Machi 19, 2024 Mkoani Arusha, Mkuu wa Operesheni za kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Nasoro Sisiwayah amesema, kikosi hicho kinaendelea kuwakamata wale wote walio kaidi agizo la kuondoa namba zenye ujazo 3D na ving’ora.

Amesema, operesheni hiyo imelenga pia kukamata madeni ya wale wote waliofanya makosa barabarani na kupigwa faini ambapo amebainisha kuwa zoezi hilo linaendela nchi nzima, huku akiwaomba watumiaji wa vyombo vya moto ambao wanadaiwa kuhakikisha wanalipa madeni yao kwa wakati.

Baadhi ya madereva licha ya kupongeza operesheni hiyo, pia wamebainisha kuwa uondoshaji wa namba hizo utasaidia katika suala la ulinzi na usalama, huku wakiliomba Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kuendelea na operesheni hiyo.

IRUWASA yaandika historia mpya, yabeba tuzo mshindi wa kwanza
DKT. Biteko ashiriki sherehe za kusimikwa Askofu mpya Mafinga