Rais wa FC Barcelona, Joan Laporta, amesisitiza kuwa kiungo Frenkie de Jong hana nia ya kuondoka klabuni hapo kwenye dirisha linalokuja la usajili wa majira ya kiangazi.

De Jong amekuwa mchezaji muhimu kwa Barca tangu uhamisho wake wa euro milioni 75 kutoka Ajax mwaka 2019.

Lakini thamani yake kubwa imekuwa ikimfanya kuwa mtaji, licha ya matatizo makubwa ya kifedha ya klabu hiyo na Barca walijaribu kumbakiza Mholanzi huyo ambaye awali alikuwa akiwaniwa na Manchester United karibu miaka miwili iliyopita.

Licha ya Wakatalunya wakiwa bado hawajaondoka kwenye hali mbaya ya kifedha, mustakabali wa De Jong na wale wengine kadhaa akiwamno Ronald Araujo na Pedri bado haujajulikana, ingawa mchezaji mwenyewe amekuwa akisisitiza kwamba anataka kubaki na Laporta amethibitisha kwamba bado haijabadilika.

“Ana furaha akiwa Barcelona. Kitu cha mwisho ambacho angetaka ni kuondoka Barcelona. Ameniambia zaidi ya mara moja, kwamba amefurahishwa hapa,” alisema rais huyo akiliambia gazeti la Mundo Deportivo.

“Tuna nafasi ya mkataba mpya. Tumefurahishwa naye,” aliongeza Laporta.

“Sina wasiwasi na mtu yeyote na kama mtu anataka kuondoka, hatuwezi kwenda kinyume na matakwa ya mchezaji. Lakini nadhani kila mtu anataka kubaki na tunataka kila mmoja wetu abaki.”

Manchester United waliendelea kumtaka De Jong, ambaye alikuja kujulikana Ajax chini ya Erik ten Hag, majira ya joto yaliyopita, wakati Bayern Munich pia waliuliza wakati huo.

Amekuwa akihusishwa mara kwa mara na Paris Saint-Germain, huku tetesi za Chelsea pia zikiibuka tena hivi karibuni.

Mkataba wa De Jong huko Barcelona, uliotiwa saini mwaka 2020, utaendelea hadi mwisho wa msimu wa 2025/26.

Baada ya ada kuafikiwa kati ya klabu, kilichokatisha tamaa ya uhamisho wa kwenda Manchester United msimu wa majira ya joto wa 2022 baada ya kuwasili kwa Ten Hag ni ukosefu wa ufafanuzi juu ya nani atamlipa mchezaji huyo deni lake la mshahara uliosimamishwa na Barca.

Rulani Mokwena aishtukia Young Africans
Meneja asimamishwa kazi, Usuaji mradi wamsikitisha Dkt. Biteko