Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo, Othman Masoud Othman, amewataka Viongozi wa chama hicho katika ngazi mbalimbali kujitahidi kuwa sauti ya Wananchi kwa kuibua matatizo yanayowakabili na kuyawasilisha, ili Serikali iweze kuchukua hatua.

Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo Shakani Wilaya ya Magharibi B Unguja alipofanya majumuisho ya ziara yake ya kuwatembelea wagonjwa, vizuka na wenye shida mbali mbali ikiwa ni utaratibu wa chama hicho, uliowekwa na mtangulizi wake marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.

Amesema, katika ziara hiyo ameweza kushuhudia matatizo na changamoto kadhaa ya Wananchi ambayo amejifunza yanahitaji kusimamiwa na Viongozi katika ngazi mbali mbali hasa kutokana wengi wao wanaishi katika maisha duni.

Amesema, wajibu wa Viongozi ni kushirikiana ili kuona matatizo ya Wananchi walionayo hivyo waweke mikakati na mipango mbali mbali iliyosahihi na kufanya kazi ya kuwa sauti ya Wananchi, katika kuzifikia na kuzitatua katika maeneo wanayoishi.

Simulizi: Karibia nijiue kisa masomo ya Chuo Kikuu
Ziara ya Kikazi: Waziri wa Mambo ya Nje Hungary awasili Nchini